Mark 14:55-64

55 aViongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi
Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.
lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote.
56Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana.

57Ndipo wengine wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo dhidi yake, wakisema: 58 c“Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitalibomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga jingine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” 59Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukukubaliana.

60 dBasi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” 61 eLakini Yesu akakaa kimya, hakusema neno lolote.

Kuhani mkuu akamuuliza tena, “Je, wewe ndiwe Kristo,
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?”

62 gYesu akajibu, “Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”

63 hKuhani mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? 64 iNinyi mmesikia hayo makufuru. Uamuzi wenu ni gani?”

Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo.
Copyright information for SwhNEN